MAN CITY YALIANZISHA TENA ARSENAL KUHUSU SANCHEZ

KLABU ya Manchester City imeanza kuikera timu ya Arsenal baada ya kuweka mezani ofa ya pauni mil 20 ili kuinasa huduma ya Alexis Sanchez.

Guardiola anataka kufanya usajili huo katika dirisha dogo la Januari akijua wazi mkataba wa Sanchez utakuwa ukingoni.


Katika dirisha lililopita, Sanchez alikuwa akielekea kusaini kandarasi Manchester City kabla ya mpango huo kuharibika hatua za mwishoni.

No comments