MARCO REUS AZIGONGANISHA MAN UNITED, ARSENAL

KLABU ya Manchester United na Arsenal zinapigana kuwania saini ya mshambuliaji, Marco Reus mwenye miaka 28.

Mshambuliaji huyo wa timu ya Borussia Dortmund anaweza kupatikana kiurahisi baada ya kumalizika kwa msimu huu hivyo klabu za England zinataka kutumia fursa ya kusuasua kwake kuongeza mkataba mwingine.


Klabu ya Man United inatajwa kuwa kwenye nafasi kubwa ya kumsajili baada ya kuanza mbio hizo tangu wakati wa dirisha kubwa la usajili msimu uliopita.

No comments