Habari

MANCHESTER UNITED HATARINI KUMKOSA LUKAKU KWA MAUMIVU YA ‘ENKA’

on

Romelu Lukaku amefanyiwa uchunguzi na madaktari wa Ubelgiji Jumatatu baada ya kuripoti kambi ya timu ya taifa huku akiwa na maumivu ya kifundo cha mguu. 
Mshambuliaji huyo wa Manchester United ambaye tayari ameshapachika mabao 15 msimu huu kwa klabu na kwa nchi yake, alipata maumivu ya kifundo cha mguu Jumamosi katika mchezo wa Premier League ulioshuhudia timu yake ikiichapa  Crystal Palace 4-0 na hadi sasa hajashiriki mazoezi ya timu ya taifa.
Taarifa rasmi ya chama cha soka cha Ubelgiji imesema: “Romelu Lukaku amefanyiwa  MRI Scan lakini hakuna mpasuko wala uharibifu ulioonekana. 
“Siku chache zijazo atafanya mazoezi binafsi. Hata hivyo ni mapema sana kusema kuwa hatakuwa fiti kwa michezo dhidi ya Bosnia na Cyprus”.
Hofu imetanda kwa mashabiki wa Manchester United ambao wanaamini iwapo mshambuliaji huyo atajilazimisha kuichezea timu ya taifa, huenda akatonesha mavivu na kuwa tatizo kubwa zaidi.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *