MANCHESTER UNITED YAENDELEA KUHUSISHWA NA MESUT OZIL


MANCHESTER UNITED imeendelea kuhusishwa na uhamisho wa kiungo mshambuliaji wa Arsenal Mesut Ozil.

Gazeti la Manchester Evening News limedai United ni moja ya vilabu vitatu vikubwa vinavyowania saini ya nyota huyo wa Kijerumani.

Vilabu vingine vinavyotajwa katika dili hilo linalotarajiwa kufanyika mwezi Januari, ni Real Madrid na Barcelona.

Arsenal bado haifikia muafaka wa dili jipya na Ozil, hali itakayomfanya mchezaji huyo andoke kwa usajili huru majira ya kiangazi.

No comments