MANCHESTER UNITED YAICHAPA SWANSEA 2-0 NA KUTINGA ROBO FAINALI YA CARABAO CUP ...Lingard nyota wa mchezo


Mabingwa watetezi wa Kombe la Carabao (Capital One), Manchester United wametinga hatua ya robo fainali baada ya kuwachapa Swansea 2-0.

Kocha Jose Mourinho ambaye aliwarejesha uwanjani wachezaji wake nane walioshiriki mchezo wa Premier League
wa kichapo cha 2-1 kutoka kwa Huddersfield Jumamosi iliyopita, akashuhudia timu yake ikitandaza soka safi na kupata bao moja katika kila kipindi.

Jesse Lingard ndiye aliyekuwa shujaa katika mchezo huo ambapo alifunga mabao yote katika dakika ya 21 na 59.

Beki kinda Axel Tuanzebe naye alitakata vilivyo, hali iliyotoa ishara ya kuongezeka ushindani wa kugombea namba kwenye safu ya ulinzi ya Manchester United.

SWANSEA CITY (4-5-1): Nordfeldt 6.5; Rangel 6, van der Hoorn 6, Mawson 6.5, Olsson 6 (Naughton 39 5.5); Routledge 6, Ki 7.5, Mesa 5.5 (Fer 67 6.5), Clucas 6.5, Ayew 6; McBurnie 6.5 (Abraham 72 6)

MANCHESTER UNITED (3-5-2): Romero 6.5; Lindelof 6.5, Smalling 6, Tuanzebe 7; Darmian 6.5, McTominay 6, Herrera 7.5 (Matic 66 6), Lingard 8, Blind 6.5; Rashford 7 (Lukaku 66 6), Martial 6.5 (Shaw 87)No comments