MANCHESTER UNITED 'YATENGA' PAUNI MILIONI 170 KUMTWAA HARRY KANE


Manchester United imemfanya Harry Kane kuwa lengo lake kuu la usajili wa kiangazi kijacho ambapo itakuwa tayari kuchuana na Real Madrid.

Habari kutoka Hispania zinasema Real Madrid tayari imejiandaa na mazungumzo juu ya mshambuliaji huyo wa Tottenham kwa ofa inayokisiwa kufikia pauni milioni 170.

Kwa mujibu wa The Sun la Uingereza, Manchester United ipo tayari kuweka mezani kiasi hicho cha pesa huku kocha Jose Mourinho akiwa 'shabiki' wa muda mrefu wa mshambuliaji huyo.
No comments