MAPACHA WATATU YA CHOKORAA SASA YAJA NA OFA YA MBEGE KWENYE SHOW YAO …Ubunifu mpya kabisa


Ukisikia kuishi kwingi ni kuona mengi ndiyo kama hivi. Mapacha Watatu Original chini ya Chokoraa yaja na ubunifu mpya kabisa.

Naam, kwamba baada ya show za kiingilio kinywaji chako, sasa unapewa na ofa ya mbege juu yake.

Saluti5 imetaarifikiwa kwamba show ya Mapacha Watatu Original kila Jumapili ndani ya Sam Pub, Ubungo Kibo, jijini Dar es Salaam, itakupa vitu viwili kwa mpigo.

Kwanza utapata fursa ya kuona show bure kabisa bila kiingilio chochote, pili kwa wale watumiaji wa pombe za jadi, watapewa ofa ya mbege. Dansi letu linajua lenyewe linapoelekea.


No comments