MARCUS RASHFORD AIBEBA MANCHESTER UNITED … CSKA Moscow yachapwa na Basel


Marcus Rashford ameifungia Manchester United bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Benfica ya Ureno katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, kundi A.

Bao hilo lilikuja dakika ya 64 kufuatia makosa ya kipa Mile Svilar ambaye alipiga hesabu mbovu na kujikuta anaudakia ndani ya wavu mpira wa free-kick uliopigwa na Rashfrod.

Katika mchezo mwingine wa kundi A, CSKA Moscow ilichapwa 2-0 na Basel.

No comments