MARK BAND YA RASHID PEMBE SASA SLIP WAY KILA ALHAMISI

MARK International Band inayoongozwa na nguli wa kupuliza Domo la Bata, Rashid Pembe “Professor” limebainisha kuwa kuanzia sasa litakuwa likitumbuiza ndani ya Slip Way kila Alhamisi.

Pembe ameiambia Saluti5 kuwa, katika shoo hiyo itakayokuwa ikidondoshwa kuanzia mishale ya saa 1:00 jioni na kuendelea hadi majogoo, bendi yake itahakikisha inakonga vilivyo nyoyo za mashabiki watakaokuwa wakihudhuria.

“Tunawakaribisha mashabiki wetu wote katika shoo hiyo ambayo itaanza Alhamisi ijayo ambapo tutakuwa tukiporomosha muziki wa aina zote ikiwemo Jazz, Blues, Reggae, Country, Chacha, Rock na mingineyo mingi,” amesema Pembe.


Kabla ya kuanzisha bendi hiyo ya kwake binafsi, Pembe amewahi pia kuzitumikia kwa muda mrefu bendi za Polisi Vangavanga na Vijana Jazz Band zilizochangia kumpatia umaarufu mkubwa.

No comments