MASHAUZI CLASSIC KUREJEA MANGO GARDEN KWA KISHINDO ALHAMISI HII


Kundi kabambe la miondoko ya taarab, Mashauzi Classic chini yake Jike la Simba Isha Mashauzi, Alhamisi hii linarejea kwa usongo mkubwa Mango Garden Kinondoni.

Mashauzi Classic haijatumbuiza Mango Garden tangu mwezi Septemba kufuatia ‘sintofahamu’ ya bomoa bomoa inayonukia kwenye ukumbi huo.

Hata hivyo meneja wa Mashauzi Classic Ismail Rashid “Sumaragar” ameiambia Saluti5 kuwa Alhamisi hii wanarejea Mango Garden na wataendelea kutumbuiza hapo kila Alhamisi angalau kwa mwezi wote wa Oktoba.

Sumaragar amesema bendi yao imedhamiria kukata kiu ya wana wa Kinondoni ambao hawajaiona Mashauzi Classic kwa muda mrefu.

No comments