MASHAUZI CLASSIC YAENDA KUWASHIKA MOSHI, ARUSHA NA BABATI WIKIENDI HII


Kundi la Mashauzi Classic, wikiendi hii litakuwa katika miji ya Arusha, Moshi na Babati ambapo litaporomosha burudani ya kufa mtu.

Mashauzi Classic inayoongozwa na Isha Mashauzi “Jike la Simba” itaanza mashambulizi yake mjini Arusha Ijumaa hii katika ukumbi wa Triple A.
Jumamosi Oktoba 28, Mashauzi watajitosa katika ukumbi wa Aventure mjini Moshi wakati Jumapili itakuwa ni zamu ya wakazi wa Babati kupitia ukumbi wa River Nile.

Kubwa katika ziara hii, ni utambulisho wa nyimbo mpya ikiwemo “Thamani ya Mama” ulioimbwa na Isha Mashauzi.

Meneja wa Mashauzi Classic, Ismail Rashid “Sumaragar” ameiambia Saluti5, kuwa mbali na nyimbo mpya, kundi lake litapiga nyimbo zao zote kali.

No comments