MECHI ZA KIMATAIFA HAZIJAWAHI KUMUACHA MTU SALAMA ..FELLAINI NJE WIKI MBILI


Kocha wa Ubelgiji  Roberto Martinez amethibisha kuwa Marouane Fellaini aliumia mguu kwenye mechi ya ushindi dhidi ya Bosnia.

Kiungo huyo wa Manchester United atakuwa nje ya dimba kwa wiki mbili, hiyo ikimaanisha kuwa ataukosa mchezo wa Premier League dhidi ya Liverpool Jumamosi hii.

United itakuwa bila Fellaini huku tayari ikiwa inawakosa Paul Pogba na Michael Carrick.

Mbali na mechi ya Anfield, Fellaini pia ataukosa mchezo wa ugenini dhidi ya  Benfica katika Champions League,  Huddersfield kwenye Premier Legaue na  Swansea katika Carabao Cup.
No comments