MGONJWA WA KANSA ANUNUA TIKETI 26 ZA SHOO YA LADY GAGA

MELISSA Anne Dabas, mwanamama wa Marekani ambaye alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kansa, ameamua kununua tiketi 26 za kuhudhuria tamasha la Lady Gaga akisherehekea kupona kwake.

Melissa ambaye ni shabiki mkubwa wa Lady gaga, anatarajia kushiriki kwenye tamasha la Novemba 19, mwaka huu katika jiji la Washngton DC.

Tiketi hizo 26 mama huyo amepanga kuzigawa kwa watu waliokuwa wakimsaidia kupambana na tatizo la kansa, wakiwemo watoto wake wawili, madaktari na wauguzi.

Mwanamke huyo pia amepanga kuanzisha mfuko maalum kwa ajili ya kuchangia fedha ili kusaidia matibabu kwa watu wenye matatizo ya kansa ya matiti.

No comments