MICHELLE OBAMA “AVAMIA” TAMASHA LA BRUNO MARS

MICHELLE Obama ambaye ni mke wa Barack Obama amehudhuria tamasha lililo andaliwa na Bruno Mars katika jiji la Washington DC akiwa peke yake bila kuambatana  na mzazi mwenzie.

Katika tamasha hilo ambalo lipo chini ya ziara ya “24K Magic Word Tour” Michelle alienda akiwa na zawadi maalum kwa Bruno Mars mwenye miaka 31.

Michelle alikabidhi fulana yenye maandishi “Obama 24K in Gold” ikiwa imetoka moja kwa moja kwa Obama kama zawadi.

Baada ya tukio hilo, Bruno Mars aliandika kwenye akaunti yake ya Instagram: “Usiku wa jana mama Obama amehudhuria shoo yangu na ametubariki wote tuliokuwapo ukumbini.”


Mwimbaji huyo amekuwa karibu na Obama kwa muda mrefu na kuna wakati aliwahi kufanya onyesho Ikulu ya Marekani wakati alipokuwa madarakani.

No comments