MINO RAIOLA ASEMA IBRAHIMOVIC BADO ANA MIAKA SITA ZAIDI DIMBANI

WAKALA Mino Raiola amesema kuwa mshambuliaji wa timu ya Manchester United, Zlatan Ibrahimovic mwenye miaka 36, bado ana muda mrefu wa kuendelea kucheza.

Wakala huyo amesema kuwa Zlatan bado anaweza kucheza kwa miaka mitano mpaka sita kabla ya kutundika daruga.


Mshambuliaji huyo aliongezewa muda wa kuendelea kuitumikia Manchester United baada ya kupata jeraha msimu uliopita katika michuano ya Kombe la Europa.

No comments