MKAZI WA DODOMA HII NDIYO RATIBA YA BENDI YAKO PENDWA SKY MELODIES


Kwa wale wakazi wa Dodoma na hata wageni wanaotua mji huo kila wiki, burudani safi inayowahusu ni ile itakayomiminwa na Sky Melodies.

Hii ni moja ya bendi bora kabisa mjini Dodoma ikiwa inaongozwa na mwimbaji na mtunzi Nicco Millimo.

Kila Jumatano Sky Melodies hujitosa ndani ya Ngalawa Bar inayopatikana katika hotel ya Royal Village maeneo ya Area D.

Ijumaa  hii na kila Ijumaa Sky Melodies ambayo inatesa na wimbo wao mpya “Hapa Kazi Tu”, wanapatikana Nkuhungu Le Chasa Nkuhungu wakati Jumamosi zote wanatumbuiza Belafonte Pub jirani na NK Disco.

Kila Jumapili Sky Melodies hukamilisha wiki kwa show matata ndani ya Club la Aziz – Makole.


No comments