MKUDE, MNYATE SASA MAMBO SAFI SIMBA SC

WACHEZAJI wawili waliokuwa wanasugua benchi katika kikosi cha Simba tangu kuanza kwa Ligi msimu huu, Jonas Mkude na Jamal Mnyate wana uhakika wa kuwa miongoni mwa kuwa kikosi cha kwanza cha Simba, imefahamika.

Chanzo kimoja kinasema kwamba kocha mkuu wa Simba raia wa Cameroon, Joseph Omog amevutiwa na kiwango cha wachezaji hao na ameanza kufikilia kuwapa namba katika kikosi cha kwanza katika mechi za Ligi zijazo.

“Kocha ametumia mechi ya Dodoma FC kuwapima wachezaji wake, lakini amevutiwa sana na viwango vya Mnyate na Mkude na anataka kuwapa namba katika mechi zijazo” chanzo hiko kinasema.


Habari hizo zinasema kwamba anachofanya sasa ni kuangalia namna gani ataweza kuwapa nafasi ya pamoja James Cotei ambaye anacheza kwa kiwango cha juu na Mkude kwa pamoja, lakini pia namna ya kuwatumia Emanuel Okwi na Mnyate kwa pamoja.

No comments