MOURINHO AKOMAA KWA BEKI DANNY ROSE WA TOTTENHAM

KOCHA wa timu ya Manchester United, Jose Mourinho bado hajakata tamaa ya kumsajili beki wa kushoto wa timu ya Tottenham, Danny Rose mwenye miaka 27.

Klabu ya Spurs imeweka kipengele cha kumuuza beki huyo kwa pauni mil 50 kwa klabu yoyote inayomtaka.


Manchester United bado haijapata namba tatu wa uhakika na Jose Mourinho anaweza kuingia sokoni kwa nguvu kwenye dirisha dogo la usajili Januari.

No comments