Habari

MOURINHO ANA LAKE JAMBO KWA ANTONIO VALENCIA

on

JOSE MOURINHO atachagua mechi za kucheza  Antonio Valencia msimu huu.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ecuador amefanikiwa kujenga himaya kwenye mipango ya Mourinho akicheza kama beki wa kulia.
Valencia mwenye umri wa miaka 32, amecheza mechi zote saba za Premier League msimu huku United ikishinda mara sita na kutoa sare mchezo mmoja.
Kwa mujibu wa ESPN, Mourinho sasa atadhibiti idadi ya mechi atakazocheza Valencia msimu huu.
Mourinho anataka  kuhakikisha Valencia anakuwa fiti kwa mechi zote muhimu huku akiamini kuwa kumpunguzia baadhi ya mechi kutasadia kumlinda beki huyo na majeraha.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *