MOURINHO: MKALI WENU IBRAHIMOVIC ANAKUJA KUWASHIKA


Jose Mourinho anaamini Zlatan Ibrahimovic atarejea uwanjani kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Nyota huyo wa Sweden amerejea Carrington (uwanja wa mazoezi wa United) wiki kadhaa zilizopita  na tayari ameanza mazoezi mepesi.

Ibrahimovic ambaye anapona kwa haraka sana, anatarajiwa kuanza kuitumikia United mapema mwezi Disemba huku mechi yake ya kwanza ikirajiwa kuwa dhidi ya CSKA Moscow katika  Champions League 


No comments