MSAFIRI DIUOF HAJUI MAFANIKIO YA CHRISTIAN BELLA …awataka wasanii wa dansi wa-relax


Mwimbaji na rapa staa wa muziki wa dansi, Msafiri Diouf ameonyesha kuwa hana analojua kuhusu mafanikio ya Christian Bella kwa soko la hapa nyumbani.

Akiongea na kipindi cha Afro TZ cha Radio One, Jumatatu usiku, Diouf akadai hajui kama Bella ndiye kinara wa muziki wa dansi kwa sasa, lakini akasema kama hali ndiyo iko hivyo basi si vibaya wasanii wa dansi wakajifunza kupitia kwa Christian Bella.

Mtangazaji wa kipindi hicho, Rajab Zomboko alimuuliza Diouf kama kuna ubaya wa kwa wasanii wa dansi kutafuta ushauri kutoka kwa Bella kwa vile kwa sasa yeye ndiye mpango mzima sokoni.

Diouf akasema: “Sijui kabisa kama Bella ndiye mwenye mafanikio zaidi, hata hizo habari za kwamba show zake ndiyo zinajaza zaidi nilikuwa sijui, sikuwahi kusikia.

“Lakini kama ndiyo hivyo, sio vibaya kupata ushauri wake, ni kitu kinachokubalika kwa wasanii kubadilishana uzoefu”.

Aidha, Diouf aliwataka wasanii na wadau wa muziki wa dansi wasitaharuki kwa anguko la muziki huo kwa vile ni upepo ambao utapita.

“Wasanii wa-relax, wasipanic, watulie kabisa, haya ni mambo ya kupita”, alisema Diouf.

No comments