MSHAMBULIAJI CENK TOSUN WA BESIKTAS ANUKIA CRYSTAL PALACE

MSHAMBULIAJI wa timu ya Besiktas, Cenk Tosun anawindwa na Crystal Palace ambayo inasaka suluhu ya kuboresha safu yake butu ya ushambuliaji.

Cent Tosun mwenye miaka 26, anatajwa kuwa na thamani ya Euro mil 25, lakini Palace wapo tayari kutoa Euro mil 22.45.


Palace imekuwa na mwenendo mbovu kwenye Ligi Kuu ya England huku ikiwa inaruhusu idadi kubwa ya mabao katika mechi zake.

No comments