MSUVA AZIDI KUFANYA MAMBO "ADIMU" DIFAA HASSAN EL JADIDA... atupia bao muhimu la ugenini

WINGA wa kimatyaifa wa Tanzania Simon Msuva juzi ameifungia timu yake, Difaa Hassan El- Jadida bao muhimu la ugenini ikifungwa 2-1 katika mchezo wa Kombe la Ligi Morocco na Chabab Rif Hoceima uwanja wa Mimoun Al Arsi mjini Al Hoceima.

Kwa bao hilo, Difaa watahitaji ushindi wa 1-0 tu nyumbani kwenye mchezo wa marudiano wiki ijayo ili kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Huo ni mwendelezo wa mwanzo mzuri wa Msuva tangu ahamie timu hiyo miezi miwili iliyopita kufuatia kucheza Tanzania kwa muda mrefu.

Na hilo linakuwa bao lake la nane tangu amejiunga na timu hiyo, la pili kwenye mechi za mashindano, mengine sita akifunga kwenye mechi za kirafiki, zikiwemo za ziara ya Hispania.

Msuva alisaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na DHJ Julai 28, mwaka huu baada ya kucheza Yanga ya nyumbani, Tanzania tangu mwaka 2012 akitokea Moro United iliyokuwa tayari imehamishia maskani yake Dar es Salaam kutoka Morogoro.

Awali ya hapo, Msuva alipitia akademi ya Azam akitokea kituo cha kukuzia vipaji vya wanasoka chipukizi, wakati baada ya kuibuliwa na iliyokuwa taasisi ya Pangollin ya kocha Charles Boniface Mkwasa, ambaye sasa ni katibu wa Yanga, klabu iliyoichezea na kuifundisha awali.


Na baada ya kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na mfungaji bora mara mbili Msuva amehamia Morocco kusaka Changamoto mpya na mafanikio zaidi kisoka.

No comments