‘MZEE YUSSUF AMEONDOKA NA TAARAB YAKE’


Aliyekuwa mwimbaji na mshereheshaji (MC) wa Jahazi Modern Taarab, Mwansiti Robert, amedai Mzee Yussuf ameondoka na soko la taarab.

Akiongea na kipindi cha Sham Sham za Pwani cha ITV, Mwansiti akasema tangu Jahazi ianzishwe (miaka 11 iliyopita), hakuna mtu mwingine aliyeishika taarab kama Mzee Yussuf.

Mzee Yussuf aliamua kustaafu muziki mwaka jana na kujikita kwenye biashara zake zingine pamoja kuzama kwenye ibada.

“Hukuna msanii mwingine aliyekuwa ameibeba juu taarab kama Mzee Yussuf na simuoni sasa anayeweza kuziba pengo lake,” alisema Mwansti katika mahojiano yake na Hawa Hassan.

Mwansiti ambaye ni mtoto wa mwimbaji wa zamani wa taarab marehemu Leyla Hatib, akasema kwa sasa anashindwa kuipa namba moja Jahazi Modern Taarab kwenye soko la taarab.

“Naweza kuipa namba moja kwa vile bado inabebebwa na nyimbo za zamani, lakini pia naweza kuinyima namba moja kwa kuwa ziko bendi nyingi zinazojitahidi kufanya vizuri kupitia nyimbo mpya,” alisema Mwansiti ambaye kwasasa amepumzika kujishugulisha muziki.
Mwansiti Robert


No comments