NICKI MINAJ AKANA "KUCHEPUKA" NA NAS

RAPA mtukutu, Nicki Minaj amekanusha uvumi unaomuhusisha kutembea na mkongwe wa HipHop, baada ya wawili hao kuanza kuonekana wakiwa pamoja maeneo mbalimbali.

Nicki hivi karibuni alipigwa picha akiwa na Nas kwenye mgahawa wa Sweet Chick wakiponda raha, hali iliyochochea uvumi huo.

Katika mahojiano yake, Nicki amesema kwamba kwake ni faraja kukaa na staa mkubwa wa HipHop kama Nas na mengine yote yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii yanabaki kuwa uvumi tu.


“Yeye ni mfalme wa HipHop na mimi ni malkia, sasa kuna tatizo gani nikiwa nae pamoja kwa mazungumzo na kupiga picha,” ilisomeka taarifa fupi aliyoituma kwenye mtandao wa kijamii.

No comments