"NIMEPIGA KOLABO ZAIDI YA 600, UTANIWEZA WAPI?" MR BLUE ATAMBA

MSANII wa muziki wa bongofleva, Mr Blue amesema amefanya kolabo takriban 600.

Kauli ya msanii huyo inakuja mara baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa kuna baadhi ya mistari yake imekuwa ikijirudia kwenye baadhi ya ngoma anazoshirikishwa, hasa na wasanii chipukizi.

Akiongea na eNews ya EATV, Blue amesema kuwa hilo linaweza kutokea kutokana na wingi w a kazi anazozifanya.
“Juzi tulikuwa tunahesabu na watu, nimefanya kolabop karibia 600 na washikaji tangu nimeanza gemu,” amesema Mr Blue.

“Kwa hiyo kurudia sometimes inaweza ikatokea kwasababu sijui niliimba kwa nani na nani, kwa hiyo inatokea kama binadamu,” ameongeza.

No comments