NIYONZIMA AOMBA MUDA ZAIDI SIMBA SC

KIUNGO fundi wa Simba na nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda, Haruna Niyonzima “Farbegas” amedaiwa kuomba muda upya wa kujifua ili kuwa katika hali yake ya kawaida.

Habari zinasema kwamba Haruna ameambiwa makocha wa Simba kwamba anataka kujinoa zaidi na kwamba ikibidi wameweke benchi kwanza kwenye mechi kadhaa hadi awe timamu zaidi.

Chanzo kimoja kinasema kwamba ni kweli Haruna anataka muda wa kujiweka fiti zaidi kwani amekuwa akicheza chini ya kiwango chake, hata hivyo sababu kubwa ikiwa ni majeruhi na baadaye kupatwa na homa.

“Ni kama Haruna hataki kabisa lawama kwenye mechi ijayo ya Yanga, anataka kucheza akiwa fiti kwa asilimia 100 ili awaoneshe Yanga kwamba kuchoma jezi yake walikuwa wanampa Baraka zaidi.” 

“Unajua Haruna ni mchezaji anayejitambua. Sio kwamba analilia tu kucheza, lakini ameona kwamba kuna tatizo kwake. Anachofanya sasa ni kujiweka fiti zaidi ili aweze kusaidia timu,” kimesema chanzo hicho.

Baadhi ya mashabiki wa Simba wamekuwa wakisema kwamba kocha wa Simba amekuwa akichezesha Mnyarwanda huyo huku akiwa hajawa timamu na kumfanya kucheza chini ya kiwango.

Lakini mtoa habari huyo amesema kwamba Niyonzima yeye ameomba muda wa kujifua zaidi, kwasababu hata yeye mwenyewe anaomba kwamba hayuko kwenye kiwango chake anachokitaka.

Kama kocha wa Simba, Joseph Omog atakubalina na ushauri wa Haruna maana yaani kwamba kiungo huyo anaweza kukosekana kwenye mechi mbili za Ligi Kuu, lakini anaweza kuwa timamu zaidi kwenye mechi dhidi ya mwajiri wake wa zamani, Yanga.


Kiungo huyo alisaini Simba kutoka kwa mahasimu wao wakubwa Yanga huku akiacha simanzi kubwa kwa wanajangwani hao ambao walijawa na jazba mpaka wakachoma jezi namba nane aliyokuwa akiivaa Yanga.

No comments