NYOSH EL SAADAT AWAITA TOTO TUNDU, CHACHA TUMBA KUCHOTA BUSARA ZAKE

“RAIS wa Vijana” Nyosh El Saadat ameifungulia milango bendi mpya ya muziki wa dansi ya River Music Band “kumsumbua” muda wowote endapo itahitaji ushauri kutoka kwake.

River Music iliyo chini ya Kiongozi Chacha Tumba na ambayo maskani yake makuu ni Kibaha Picha ya Ndege, inakusanya wasanii wengi mahiri waliowahi kutamba na bendi nyingine huko nyuma, akiwemo Mhina Panduka “Toto Tundu”.

Hivi karibuni Nyosh aliitembelea bendi hiyo na kushiriki nao shoo moja ndani ya ukumbi wao wa nyumbani wa River Road Bar ulioko Kibaha Picha ya Ndege, ambapo alionyesha kuukubali vilivyo uwezo wa wanamuziki wake.


“Nawakaribisha sana wadogo zangu akina Chacha Tumba, Toto Tundu na wote mnaounda bendi hii kwa msaada wa ushauri wa kimuziki na mambo mengine mbalimbali, msisite njooni tu mimi ni rais wa wasanii bwana,” amewaambia Nyosh.

No comments