NYOSHI KUSAHAULIKA FM ACADEMIA BADO SANA


Ni zaidi ya miezi mitatu sasa tangu Nyoshi el Saadat ajiengue FM Academia, lakini bado wadau wa muziki inawawia vigumu kumtenganisha mwimbaji huyo na bendi yake hiyo ya zamani.

Sura ya Nyoshi ambaye hadi sasa anaendelea kujipanga kimya kimya na ujio wa bendi yake mpya, imeendelea kutumika kwenye baadhi ya matangazo (posters) ya kunadi show za FM Academia.

Mengi kati ya matangazo hayo  ni yale ambayo yanaandaliwa na mapromota wanaoikodi bendi ambapo kwa makusudi au bahati mbaya, wamekuwa wakiweka picha ya Nyoshi kwenye matangazo hayo.

Miongoni mwa matangazo hayo ni pamoja na lile la uzinduzi ukumbi mpya wa Rufita Park ulioko Segerea, show iliyofanyika jana Ijumaa huku watumbuizaji wakuu wakiwa ni FM Academia.

No comments