Bosi wa bendi ya mipasho, Ogopa Kopaz Classic Band, Khadija Kopa ameizungumzia shoo yao maalum iliyopangwa kudondoshwa Ijumaa hii ndani ya Travertine Hotel, jijini Dar es Salaam na kusema kuwa anavyoamini itakuwa funika bovu.

Akiongea na Saluti5, Kopa amesema kuwa anaamini hivyo kutokana na maandalizi makubwa waliyoyafanya, ikiwemo kuwaalika wasanii kumi wa miondoko tofauti tofauti ya muziki hapa Bongo.


Shoo hiyo iliyopewa jina la “Usiku wa Ishu Pambe”, itaanza kuunguruma majira ya saa 3:30 usiku na kuendelea hadi majogoo, ambapo burudani kutoka kwa Hanifa Maulid, Kivurande Junior, MC Sudi na matarumbeta, zinatarajiwa kunogesha.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac