Manchester United ipo kwenye mipango ya kuutanua uwanja wa Old Trafford hadi kufikia uwezo wa kuingiza watu 88,000.

Mapendekezo hayo ya kuongeza zaidi ya viti 12,000 kutoka kwenye jumla ya viti 75,643 vya sasa, yatafikiwa kwa kupanua jukwaa la Sir Bobby Charlton ambalo zamani lilikuwa likijulikana kama South Stand.

Upanuzi huo  unaotarajiwa kukamilika 2020, utaifanya Old Trafford kupiku viwanja vya San Siro, Bernabeu, Stade de France na Westfalenstadion na kwa Ulaya itakuwa nyuma ya Wembley yenye viti 90,000 na Nou Camp ya Barcelona inayochukua watu 99,354.

USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac