OMOTOLA JALADE AANIKA MAZITO ALIYOPITIA KWENYE MAISHA YAKE

STAA wa filamu mwenye mvuto wa mapenzi nchini Nigeria, Omotola Jalade Ekeinde amesema kuwa amepita wakati mgumu baada ya kupoteza baba yake mzazi akiwa na umri mdogo.

Staa huyo amesema kuwa kifo cha baba yake kilitokea akiwa na umri wa miaka kumi, hali iliyosababisha kuathiri mwenendo wa maisha yake ya shule.

“Nililazimika kuanza kujitafutia fedha nikiwa na umri wa miaka 15, sikuwa na jinsi kwa sababu nilihitaji matumizi binafsi na ada za shule,” alisema mrembo huyo.

“Nakumbuka kuna wakati nilisaidiwa na kundi la wanaume ambao walikuwa na uhusiano mzuri na baba yangu, lakini nadhani yale matatizo ndio yamechangia mimi leo kuwa na mafanikio,” ameongeza.


Omotola ameeleza hayo katika jiji la lagos wakati alipokuqwa akiwatia moyo wanawake kupambana na changamoto za kimaisha bila kukata tamaa.

No comments