OZIL AANZA KUAGA WACHEZAJI WENZIE ARSENAL

KIUNGO wa timu ya Arsenal, Mesut Ozil mwenye miaka 29 anasemekana ameanza kuaga wachezaji wenzie kufuatia mpango wake wa kuondoka London kwenye dirisha la Januari.

Ozil anahusishwa na usajili wa kwenda Manchester United ambayo ilianza kumfuatilia tangu wakati wa dirisha kubwa lililopita.


Mkataba wa staa huyo wa Ujerumani unamalizika mwishoni mwa msimu huu na hivyo kama Arsenal haitampiga bei dirisha la Januari basi ataondoka bure dirisha la kiangazi.

No comments