P. DIDDY AOTA KUMILIKI LIGI YA MCHEZO WA KIKAPU

STAA wa Hip Hop P. Diddy amesema kuwa moja kati ya ndoto zake ni kumiliki Ligi ya mchezo wa kikapu.

Suala hilo limeibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya mashabiki wakiamini inawezekana ni utani wa mitandaoni.

“Nilikuwa na ndoto ya kumiliki timu ya mchezo wa kikapu lakini sasa nina ndoto ya kumiliki Ligi yangu!” ilisomeka sehemu ya taarifa iliyotumwa na rapa huyo tajiri duniani.


“Huu ndio mpango wangu sasa kuwa na kitu changu kwenye mchezo wa kikapu najua ni wachache wanawaza kama mimi,” aliongeza.

No comments