PICHA 10: BELLA ALIVYOJUA NINI MASHABIKI WA DODOMA WANATAKA TANZANIA BAND FESTIVAL


Ni kama vile mashabiki wengi walikuwa wanasubiri kupanda kwa Bella jukwaani sambamba na kundi lake la Malaika Band ambapo Kisasa Capetown Complex ikalipuka kwa furaha pale tu sauti ya mkali huyo ilipoanza kusikika kwenye kipaza sauti.

Bella akaanza kwa kuwaimbisha mashabiki wake vipande tofauti tofauti vya nyimbo zake. Ikawa shangwe kubwa, dancing floor ikatapika mashabiki. Baada ya hapo akaanza kushusha nondo baada ya nondo.

Nyimbo kama “Nakuhitaji” “Nani Kama Mama” na “Nishike” zilikuwa ni baadhi tu ya vitu vilivyowapagawisha mashabiki ambao walikuwa wakicheza na kuziimba nyimbo hizo kwa hisia kali.
 Kalonzo na Coco Ngemba kwenye magitaa
 Mashabiki 
 Sekedia kwenye kinanda
 Makamuzi ya nguvu
 Bella na kundi lake jukwaani
Wamama wakivamia jukwaani wakati Bella alipoimba "Nani Kama Mama"
 Baba Bomba kwenye bass
Bella akifanya yake kwa raha zake


No comments