Habari

PICHA 10 ZA SHOW YA SKY MELODIES YA DODOMA …moto wao si wa kitoto

on

Wikiendi iliyopita Saluti5 ilitembelea onyesho la moja ya bendi
maarufu za mjini Dodoma – Sky Melodies chini yake Nicco Millimo.
Onyesho lilifanyika Jumamosi usiku ndani ya Kisasa Capetown Complex,
moja ya kiwanja kipya cha burudani mjini humo.
Sky Melodies walipiga show safi wakitesa na mchanganyiko wa nyimbo zao
na zile za kunakili.
Uwezo wa wasanii wa Sky Melodies ulikuwa wa hali ya juu kuanzia wapiga
vyombo hadi waimbaji, nyimbo zote zilizopigwa zilitendewa haki.
 Amos Nabii akicharaza gitaa la solo
 Emanuel Balisidya alitesa kwa kuimba ‘copy’ za reggae
 Moja ya ala iliyotendewa haki sana na Sky Melodies ni gitaa la bass ambalo lilikung’utwa na Richard Millimo
 Kiongozi wa Sky Melodies Nicco Millimo (kushoto) akiwa na mdau Ahmed Rajab
 Mcharaza drum wa Sky Melodies
 Bongito kwenye kinanda
 Nicco Millimo na mashabiki wake. Kulia ni mdau mkubwa wa dansi Mama Igwe
 Mama Igwe akizigawa nyekundu nyekundu jukwaani
 Mmoja wa waimbaji wa Sky Melodies
Nicco Milliomo akiimba moja ya nyimbo za Sky Melodies

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *