PICHA 12 ZA YAH TMK WALIVYOITEKA BULYAGA BAR JUMAMOSI USIKU


Kundi la Yah TMK Modern Taarab, Jumamosi usiku lilifanya makubwa kwenye umbi wa Bulyaga Bar, Temeke jijini Dar es Salaam.

Umati mkubwa uliofurika ukumbini hapo, ukazuuzika kwa burudani safi kutoka kwa Yah TMK ambayo ilitesa na nyimbo zao kali.

Yah TMK ambayo hupatikana Bulyga kila Jumamosi, imefanikiwa kukifanya kiwanja hicho kiwe miongoni mwa viwanja bora vya burudani kwa namna ambavyo kinafurika mamia ya mashibiki wa taarab kila inapopiga bendi hiyo.

Wasanii kama Omar Teggo, Aisha Vuvuzela, Fatma Mcharuko na wapigaji Chid Boy, Mohamed Mauji na Mussa Mipango na wengine wengi, kwa pamoja waliunda muunganiko uliozalisha muziki mzito uliowafanya mashabiki wasiketi kwenye viti vyao.
  Kijiji kilivyokusanywa na Yah TMK Modern Taarab
Mohamed Mauji akikung'uta solo gitaa
Fatma Mcharuko mmoja wa waimbaji tegemeo wa Yah TMK Modern Taarab
Ilikuwepo pia burudani ya matarumbeta
 Pia kulikuwa na show kutoka kwa wadada wakali
Meneja wa Yah TMK, Mudd K akiongea machache 
Mussa Mipango kwenye bass gitaa
Hali ilikuwa kama hivi
Omar Teggo akifanya yake
Aisha Vuvuzela 
Chid Boy akipapasa kinanda

No comments