PICHA 16: MAPACHA WATATU ORIGINAL ILIVYOACHA SIMULIZI MJINI MOSHI

MAPACHA Watatu Original chini ya Khalid Chuma “Chokoraa” juzi Jumamosi ilisafiri hadi mkoani Kilimanjaro ilipoangusha shoo ya nguvu ndani ya Furahisha Pub, Kibosho Road na kuacha simulizi kubwa mjini Moshi.

Timu hiyo ya Mapacha watatu Original iliondoka jijini Dar es Salaam majira ya saa 5:51 usiku wa Ijumaa na kuingia mkoani Moshi mishale ya saa nne asubuhi ya siku iliyofuata ambayo ndio ilikuwa siku ya tukio.

Katika shoo hiyo iliyohudhuriwa na mashabiki wengi, Mapacha watatu Original ilionekana kutakata vilivyo, hasa kutokana na kumudu kisawasawa kukonga mioyo ya mashabiki waliokuwa wamefurika kwa vibao vyao mbalimbali kikiwemo kile kipya cha “Yananitesa”.


Waimbaji Frank Kabatano, Catherine Cindy  na Khalid Chokoraa mwenyewe pamoja na wapiga ala Evans Mwaigomole na Super Black walikuwa kivutio tosha, huku wanenguaji Sabrina Kado, Master D na Otilia Kandoro wakipagawisha kwa staili zao za kumtoa chatu nyikani. 

 Huu ndio usafiriri uliotumiwa na Mapacha Watatu Original kwenda Moshi na kurudi
Hapa safari inaanza
 Khalid Chokoraa akiwa mbele ya gari yao tayari kwa safari
 Katikati ya shoo Chokoraa akimuimbia shabiki aliyefahamika kwa jina la mama Jerome
  Catherine Cindy akiimba kwa hisia kali
 Frank kabatano akiwakoleza mashabiki 
 Mkaanga Chips Tontoo Machine akiwajibika
Chokoraa akipasua koo
Kabatano (kushoto) na Cindy wakiimba pamoja
 Evans Mwaigomole akiungurumisha gitaa la bass
 Kabatano akiwaonyesha mashabiki ujuzi wake mwingine wa kulisakata rhumba
 Mcharazaji gitaa la solo, Super Black akifanya yake
 Baadhi ya wadau wa muziki wa mjini Moshi wakichizika
 Mnenguaji Sabrina Kado akifanya yake jukwaani
 Sehemu ya mashabiki waliohudhuria
Mashabiki wakilisakata sebene la Mapacha watatu Original

No comments