PICHA 18: MASHAUZI CLASSIC WAWEKA HESHIMA ARUSHA


Kundi la Mashauzi Classic chini yake Jike la Simba - Isha Mashauzi, Ijumaa usiku lilipiga show ya kibabe ndani ya Club Triple A, Arusha na kukonga nyoyo za mashabiki wengi waliohudhuria onyesho hilo.

Waimbaji kama Asia Mzinga, Sofia, Aziza, Rahma Aman, Hashim Said na Abdumalick Shabaan, kila mmoja alitesa kwa staili yake kupitia nyimbo zao kali.

Lakini kubwa kuliko, ilikuwa ni namna Isha Mashauzi alivyoiteka show kwa kukamua zaidi ya nyimbo sita mfululizo na kuwafanya mashabiki wasiviguse tena viti vyao kwa muda wote huo.

Baadhi ya nyimbo alizoimba Isha ni pamoja na “Viwavi Jeshi”, “Mapenzi Hayana Dhamana”,  “Umdhaniaye Ndiye”, “Sura Surambi”, “Thamani ya Mama”  na “Nimpe Nani”
Asia Mzinga akiimba "Ubaya Haulipizwi"
 Kali Kitimoto kwenye kinanda
 Isha Mashauzi akipagawisha shabiki wake
 Isha Mashauzi jukwaani
 Isha Mashauzi akiendelea kuzikonga nyoyo za mashabiki wake
 Isha akifanya yake
 Mkude Simba akikamata mpini wa solo
 Umati wa mashabiki ukimwagika kwenye dancing floor
 Isha Mashauzi
 Rahma Amani 
 Rahma Amani akiimba kwa hisia
 Mwimbaji chipuki wa Mashauzi Classic Sofia Juma
 Abdumalick Shaaban jukwaani
 Shabaan wa Kumwaga kwenye bass
Waimbaji wa Mashauzi Classic
 Aziza akiimba moja ya nyimbo za Mashauzi Classic
 Hashim Said
Hashim Said akiimba "Bonge la Bwana"No comments