Habari

PICHA 38: JIKUMBUSHE TANZANIA BAND FESTIVAL YA MWAKA JANA ILIVYOKUWA NDANI YA LEADERS CLUB

on

TAMASHA la muziki wa bendi za Tanzania (Tanzania Band Festival) lililofanyika kwa mara ya kwanza Jumamosi usiku (Julai 30, 2016) katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam, lilipokewa kwa msisimko wa aina yake.
Bendi kama Msondo Ngoma, Sikinde, B Band, Akudo, FM Academia, Skylight, Twanga Pepeta, Yamoto na nyingine nyingi, zikapata wasaa wa kuonyesha ufundi wao jukwaani.
Haikuwa mashindano, bali lilikuwa ni tamasha lililodhamiria kuleta mshikamano na mingoni mwa bendi zetu, hususan zile za muziki wa dansi.
Kama mapungufu kadhaa yaliyojitokeza yatafanyiwa kazi vizuri, basi tamasha hilo ambalo limepangwa kufanyika kila mwaka, litakuwa ni jukwaa muhimu ya kuukwamua muziki wa dansi.
Waandaaji wa onyesho hilo, Q Plus General Enterprises wanapaswa kupongezwa na kuungwa mkono badala ya kukatishwa tamaa kutokana na ukweli kuwa kuzikutanisha bendi nyingi kiasi kile maana yake ni kwamba unazungumzia matumizi ya uwekezaji mkubwa wa  pesa.
Mpangilio wa show ulikuwa kama ifuatavyo: TOT Band walifuangua pazia kisha wakafuata Akudo Impact, Sikinde, QS Internationa Band, King Kiki, Family Team, Msondo, Yamoto, B Band, Top Band, Skylight Band, Mapacha Watatu, Twanga Pepeta kisha pazia likafungwa na FM Academia.
Onyesho lilianza rasmi majira ya saa 12 jioni na kuendelea hadi saa 10 za alfajiri.
Mgeni rasmi alikuwa ni mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mheshimiwa Paul Makonda ambaye alichangia zawadi ya shilingi milioni moja.

Jikumbushe picha 38 za onyesho hilo la Tanzania Band Festival lililofanyika Leaders Club, Dar es Salaam, Julai 30, 2016.
 B Band
 Shaaban Dede wa Msondo (kushoto) na Zomboko wa Radio One
 Family Team
 MC wa onyesho alikuwa ni Khamis Dacoto wa Clouds FM/Clouds TV
 King Kiki akipeperusha kitambaa cheupe na bendi yake
 Madansa wa FM katika picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda
 Madansa wa Mapacha Watatu
 Jose Mara boss wa Mapacha Watatu
 Mapacha wakikamua
 Mashabiki wakifurahia onyesho
 Khamis Dacota akimkaribisha mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda
 Mheshimiwa Makonda akizungumza machache
 Mheshimiwa Makonda akiendelea kuongea na wapenzi wa muziki
 Msondo
 FM Academia
 FM Academia wakiwa smati kwa sana
 Nyoshi rais wa FM Academia
 Hao ndiyo Wazee wa Ngwasuma bwana!
 Pangamawe wa Msondo Ngoma
 Asha Baraka (kulia) akiwa na shabiki wa muziki
 Mjusi Shemboza wa Sikinde
 Sikinde
 Skylight Band
 Akudo Impact
 Top Band
 TOT Band
 TOT Band katika ubora wao
 Madansa wa Twanga
 Ally Chocky (aliyeshika kipaza sauti) akiliongoza jahazi la Twanga
 Khalid Chokoraa wa Twanga Pepeta katika staili yake ya kipekee
 Kaposhoo kwenye tumba za Twanga
 Luizer Mbutu wa Twanga
 Twanga Pepeta wakiruka uzio kwenda kwa mashabiki
 Watangazaji wanaosaka kuwani kutangaza kipindi cha Bambataa wakisalimia jukwaani
 Yamoto Band wakiimba wimbo wa Mama
 Yamoto Band 
 Yamoto Band  wakishambulia jukwaa

Chiba wa Yamoto Band alikuwa kivutio sana

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *