PICHA 4: CHOKORAA ATANGAZA KUMNG’OA GOD KANUTI TWANGA PEPETA …mashabiki wa Mapacha washangilia


Mpiga solo wa Twanga Pepeta, God Kanuti hakusafiri na bendi yake kwenda mikoani kwenye show za Tanzania Band Festival na badala yake akashiriki kikamilifu onyesho la Mapacha Watatu Original ndani ya Brazil Pub Tegeta Ijumaa usiku.

Kanuti pia alishiriki onyesho la Mapacha Watatu Original ndani ya Meridian Hotel Kinondoni Jumatano usiku.

Ingawa habari za ndani zinasema Kanuti amekorofishana na mmoja wa maboss wa Twanga Pepeta, lakini msanii huyo akaimbia Saluti5 kuwa amebaki Dar es Salaam kwaajili ya kumuuguza mama yake.

Katika onyesho la Brazil Pub, kiongozi wa Mapacha Watatu, Khalid Chokoraa akawauliza mashabiki: “Je mnataka tumng’oe Kanuti Twanga Pepeta na kumleta Mapacha?”

Mashabiki walipoitikia ndiyo, Chokoraa akaongeza: “Niachieni hiyo kazi, nitahakikisha ninamtoa Kanuti Twanga Pepeta na kumhamishia Mapacha”.
Hata wakati Kanuti anashiriki kupiga solo kwenye wimbo “Yananitesa” na kutuzwa pesa na mashabiki, Chokoraa akatupia kijembe: “Kanuti si unaona huku unatuzwa pesa kibao, kule hutuzwi kabisa, njoo huku, mambo mazuri yako huku”.

Saluti5 ilipomfuata Chokoraa na kumuuliza kama ni kweli amedhamiria ‘kumsajili’ Kanuti, akasema ni mapema mno kusema lolote ingawa  katika muziki chochote kinawezekana.


Hata hivyo Kanuti aliiambia Saluti5 kuwa amekwenda Mapacha kusalimia kisanii na yeye bado ni mwanamuziki mtiifu wa Twanga Pepeta.
 Kapatano akimchagiza Kanuti kwenye show ya Mapacha Watatu Original
 God Kanuti kwenye jukwaa la Mapacha Watatu Original
 Kanuti (katikati) akiwa sambamba na Chokoraa na Kabatano ndani ya Brazil Pub Tegeta
Chokoraa akiwahakikishia mashabiki wake kuwa bendi yake itamsajili Kanuti

No comments