PSG MZIKI MNENE KWA ANDERLECHT …Bayern Munich 3 - 0 Celtic


Paris Saint Germain imeitandaika Anderlecht ya Ubelgiji 4-0 katika mchezo wa kundi B wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Safu kali ya ushambuliaji ya PSG imeendelea kuwa moto wa kuotea mbali ambapo washambualiaji Kylian Mbappe, Edinson Cavani, Neymar na Di Maria kila mmoja alitupia wavuni bao moja.

Katika mchezo mwingine wa kundi B, Bayern Munich ikaichapa Celtic 3-0 kupitia kwa Thomas Mueller, Joshua Kimmich na Mats Hummels.

No comments