RADIO UHURU KUWAKUSANYA MASTAA WA BONGO FLEVA, DANSI, TAARAB NA SINGELI NYERERE DAY MWEMBE YANGA


Umewahi kujiuliza itakuweje pale utakapowakusanya pamoja mastaa wa muziki wa dansi, taarab, bongo fleva na singeli halafu wakachuana jukwaa moja?

Jibu litabatikana Jumamosi ya Oktoba 14 (Nyerere Day) pale Temeke Mwembe Yanga wakati Radio Uhuru ya jijini Dar es Salaam itakapofanya tamasha kubwa la kilele cha kampeni iliyopewa jina la “Gusa Maisha Yao”.

Mmoja wa waratibu wa kampeni hiyo ambayo imelenga kutoa misaada mbali mbali kwa jamii, Kigwa One, ameiambia Saluti5 kuwa miongoni mwa bendi za dansi zitakazokuwepo Mwenye Yanga ni pamoja na Mapacha Watatu Original chini ya Chokoraa, Dar Musica chini ya Jado FFU, Double M Sound ya Mwinjuma Muumin, Msondo Ngoma na Telent Band chini ya Hussein Jumbe.

Aidha, Kigwa amesema kwa upande wa taarab watakuwepo Isha Mashauzi na Khadija Kopa na wengine wengi. Kwenye bongo fleva atakuwepo Beka Fleva, Madada Sita na Juma Nature wakati singeli itapambwa na  wakali kibao akiwemo Dulla Makabila.

Kigwa amesema tamasha hilo litaanza saa 5 asubuhi hadi saa 12 jioni.

No comments