RAPA DMX APIGANIA KUACHANA NA DAWA ZA KULEVYA

RAPA wa Hip Hop aliyewahi kutamba miaka ya nyuma kutokana na kuimba kwa sauti nzito, DMX  yupo kwenye vita kali ya kuachana na matumizi haramu ya dawa za kulevya.

DMX ambaye hivi karibuni alikumbwa na kesi ya kukwepa kodi, amekuwa akitumia muda mwingi kushinda kwenye kliniki ya tiba za kupunguza uraibu wa dawa za kulevya.

Akiwa anatoka kwenye ukumbi wa mahakama huko Manhattan nchini Marekani kwa ajili ya kujibu kesi ya kukwepa kodi, rapa huyo alidai kwamba anajisikia vizuri kuona ameanza kushinda vita ya kuachana na dawa hizo zinazopigwa marufuku ulimwenguni kote.

DMX alikuwa akituhumiwa kukwepa kodi inayokadiriwa kufikia kiasi cha dola mil 1.7 zinazotokana na kazi zake za kisanii.


Mapema mwaka huu alipimwa na kugundulika anatumia dawa za kulevya aina ya Cocaine.

No comments