REAL MADRID KAZI WANAYO MSIMU HUU LA LIGA ...waendelea kuachwa mbali na Barcelona


Real Madrid ambayo imechukua kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Girona, imejikuta iko nyuma kwa pointi inane dhidi ya vinara wa La Liga, Barcelona.

Kwa kichapo hico, Real Madrid inayonolewa na Zidane, inazidi kujiweka pabaya katika harakati zao za kutetea taji la La Liga.

Isco aliitanguliza Real Madrid kwa bao la dakika ya 12 lilolodumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili dakika ya 54 na 58 Girona wakacharuka na kupata mabao mawili ya haraka haraka kupitia kwa  Cristian Stuani na Cristian Portu.

No comments