REAL MADRID KUMALIZANA NA THIBAUT COURTOIS JANUARI MWAKANI

KIPA wa timu ya Chelsea, Thibaut Courtois raia wa Ubelgiji ameingia kwenye rada ya Real Madrid ambao wamepanga kumalizana nae katika dirisha la Januari, mwakani.

Kipa huyo amegoma kuongeza mkataba mpya na Chelsea huku akiwa anasubiria ofa ya kuhamia Hispania katika dirisha dogo lijalo.


Courtois mwenye miaka 25, anatarajiwa kumaliza mkataba wake Stamford Bridge mwaka 2019.

No comments