REAL MADRID "KUMTUPA" BENZEMA KWA AJILI YA HARRY KANE

KLABU ya Real Madid ipo tayari kuachana na mshambuliaji wake Karim Benzema mwenye umri wa miaka 29 ili kumnasa mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane.

Benzema alikuwa aondoke kwenye kikosi hicho katika dirisha kubwa la usajili msimu uliopita lakini mpango huo ulikwama dakika za majeruhi.

Real Madrid inaona njia pekee ya kumpata Kane ni kumtoa Benzema pamoja na fungu kubwa la fedha.

No comments