REAL MADRID YAJUTA KUTOMPIGA BEI GARETH BALE

KLABU ya Real Madrid imeripotiwa kujutia kitendo chake cha kutomuuza mshambuliaji wake, Gareth Bale katika dirisha kubwa lililopita.

Bale mwenye miaka 28, alitakiwa kwa ada kubwa na klabu ya Manchester United wakati wa majira ya kiangazi lakini Real Madrid hawakuwa tayari kuachana nae.


Pamoja na ubora wake, lakini hali yake kiafya imekuwa haieleweki na mara kwa mara amekuwa akipatiwa matibabu kwasababu ya majeruhi.

No comments