REAL MADRID YAPANIA KUMSAJILI CAVANI DIRISHA LA JANUARI


Real Madrid inapiga hesabu za kumsajili nyota wa PSG Edinson Cavani katika dirisha dogo la Januari.

Cristiano Ronaldo, Karim Benzema na Gareth Bale bado hawako kwenye fomu nzuri msimu huu huku Real Madrid ikishika nafasi ya tano kwenye La Liga ikiwa pointi saba nyuma ya vinara Barcelona.

Na sasa Real Madrid inaona upo umuhimu wa kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kwa kuangazia washambuliaji kadhaa akiwemo Cavani.

No comments