RONALDO SI MTU MZURI KWA MANCHESTER UNITED, ATAKA KUMNG’OA RASHFORD OLD TRAFFORD


Real Madrid itafanya juhudi za kumsajili mshambuliaji wa Englanda na Manchester United, Marcus Rashford kiangazi kijacho. 

Rashford amefanywa kama chaguo la pili ambapo iwapo rais wa Real Madrid Florentino Perez  atashindwa kumsajili Harry Kane wa Tottenham, basi hasira zao zitaelekezwa kwa kinda huyo wa United.

Mtandao wa Hispania unaojulikana kama Don Balon umeandika kuwa Rashford ni 'plan B' iwapo Kane ataamua kukutaa ofa ya kwenda Santiago Bernabeu.

Don Balon pia ikaandika kuwa Rashford ni pendekezo la mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ambaye naye pia anamuona mchezaji huyo kama chaguo sahihi baada ya Harry Kane.

No comments